Bilioni 19 za GGM kusaidia jamii Geita

0
176

Mgodi wa kuzalisha dhahabu wa Geita (GGM) umepanga kutumia shilingi Bilioni 19 kwa shughuli mbalimbali za kijamii kwenye wilaya ya Geita, Chato, Mbogwe na Bukombe.

Katika mgao huo halmashauri ya Geita Mji na Geita DC zitapata shilingi Bilioni 9.2 huku Chato, Mbogwe na Bukombe zikipata shilingi Milioni 200 kila moja.

Makamu wa Rais wa GGM anayeshughulikia uendelevu wa mgodi huo Simon Shayo amesema, fedha hizo ni kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2021/2022 na 2022/2023.

Ameongeza kuwa kwa mwaka huu wameongeza pia fedha kwa ajili ya halmashauri za wilaya za Chato, Mbogwe na Bukombe kutoka shilingi Milioni 100 kwa mwaka mpaka kufikia shilingi Milioni 200.

Shayo amesema mbali na miradi ya maji, elimu na afya GGM pia inatoa fedha kwa ajili ya kilimo cha alizeti na kuwekeza katika michezo.