Bilioni 15 kutatua migogoro ya hifadhi na wananchi

0
152

Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa na Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess wameshuhudia kusainiwa kwa mkataba wa utekelezaji wa mradi wenye thamani ya shilingi Bilioni 15.

Mkataba huo uliosainiwa mkoani Dar es Salaam, una lengo la kuisaidia Tanzania kupambana na wanyama waharibifu katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania.

Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi na Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ) kwa upande wa Tanzania.

“Kusainiwa kwa mkataba huu ni ishara kuwa Serikali imeanza na itaendelea kulipa uzito suala la uhifadhi na hasa kupunguza athari za wanyama waharibifu kama tembo kwa kushirikiana na wadau kama mnavyoona hapa leo”. Amesema Waziri Mchengerwa