Bilionea Subhash Patel afariki dunia

0
191

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya Motisun Group ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watu wenye utajiri mkubwa nchini na mfanyabiashara maarufu Subhash Patel amefariki dunia.
 
Subhash Patel ni mmiliki wa hoteli ya White Sands iliyopo jijini Dar es salaam.
 
Kwa mujibu wa jarida la Forbes lililotolewa mwezi Oktoba mwaka 2018, Subhash Patel alishika nafasi ya Saba kwenye orodha ya matajiri Wanaume nchini Tanzania.
 
Wakati wa uhai wake Subhash Patel ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa umeme, alifahamika sana kwa kuwa alisaidia miradi mbalimbali ya kijamii na aliwasaidia watu wenye shida mbalimbali.
 
Subhash Patel aliyezaliwa Agosti 13 mwaka 1946 jijini Dar es salaam,  pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).