Serikal imetoa shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi za Uhamiaji mkoani Mtwara.
Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti kuzunguka jengo hilo Kamishna msaidizi wa Uhamiaji mkoa wa Mtwara, Dismus Mosha amesema ujenzi ulianza muda mrefu lakini baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani alitoa fedha hizo kwa ajili ya kukamilisha.
Mosha amesema ujenzi wa jengo hilo ukikamilika, utaongeza ufanisi na ubora katika kufanya kazi kwa kuwa wateja wao wengi ni wale wa kufanya nao mahojiano na uchunguzi ambapo unahitajika usiri mkubwa.