Biashara ya figo ni haramu

0
378

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma Dkt. Alphonce Chandika amesema, wapo vijana wengi wanaompigia simu wakitaka kuuza figo na kuwataka waache kufanya hivyo.

Dkt. Chandika amesema endapo mtu ana ndugu mwenye uhitaji wa kiungo hicho, ipo kamati maalum yenye kuthibitisha ikiwa hakuna biashara yoyote inayofanyika kwenye upatikanaji wake.

“Sheria za nchi haziruhusu biashara za viungo [vya mwili] na kwamba uuzaji wa viungo vyovyote nchini ni haramu.” amessma Dkt. Chandika