Bi Sonia afariki Dunia

0
121

Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania Farida Sabu maarufu kwa jina la ‘Bi Sonia’ amefariki dunia.

Bi Sonia ambaye alijulikana sana kupitia kikundi cha Kaole Sanaa group amefariki leo, mjini Zanzibar ambapo alikuwa anauguzwa na mwanae.

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji, Chiki Mchoma amethibitisha taarifa hizo, huku msiba ukitarajiwa kufanyika huko huko Zanzibar.