Betri za maji mbadala wa Lithium

0
502

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Texas A&M nchini Marekani wanaendelea na utafiti ili kuja na betri inayotegemea maji na hivyo kupunguza utegemezi wa madini ya lithium kutunza nishari.

Jodie Lutkenhaus na Daniel Tabor ambao ni maprofesa katika chuo kikuu hicho wamekuwa wakitafiti juu ya betri zinazotumia maji kwa miaka kadhaa sasa, ambapo pamoja na kutumia maji baadhi ya vitu vitavyotumuka kuunda betri hizo ni “cathode, anode na eletroliti kama zilivyo katika betri za kawaida.

Betri za lithium-ion ni aina kuu za betri zinazotumika katika matumizi ya nishati ya kila siku ambapo nchi nyingi duniani huzitumia.

Kwa upande wa Marekani, watafiti nchini humo wapo na mpango wa kuhama kutoka matumizi ya lithium katika matengenezo ya Betri hata kuja na teknoojia nyingine ya betri zitazotumia maji.

Hatua hii inaleta wasiwasi wa kuwepo kwa mivutano ya kijiografia na kisiasa ambayo inaweza kuathiri upatikanaji na utoshelevu wa lithium-ion na kobalti ambayo huagizwa kutoka nje ya nchi hiyo.

Watafiti kutoka chuo hicho kikuu cha Texas A&M ni mojawapo ya vikundi nchini Marekani vinavyoungwa mkono na Idara ya nishati na Taasisi ya Sayansi ya Taifa ambapo zinatafuta mbadala wa lithium-ion katika kutengeneza betri.

Watafiti hao bado wanaendelea kuchunguza zaidi njia rafiki na mbadala ya kuunda betri zitazofanya kazi kwa ufanisi mkubwa tofauti na betri za lithium-ion.