Bei ya petroli yapanda

0
255

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya elekezi za mafuta ya petroli, dizeli na taa zitakazoanza kutumika leo Jumatano, Machi 6, 2024.

Bei za mafuta ya petroli na dizeli zimepanda kwa rejareja na jumla.

Mathalani, kwa Dar es Salaam, petroli imepanda kutoka Sh 3,051 hadi Sh 3,163.

Hii ni sawa na ongezeko la Sh 112 kwa lita. Dizeli imepanda kutoka Sh 3,029 hadi Sh 3,126, sawa ongeko la Sh 97 kwa lita.

Kwa Tanga, petroli imepanda kutoka Sh 3,064 hadi Sh 3,209.

Dizeli imefikia Sh 3,196 kutoka Sh 3,173. Mtwara petroli imefikia Sh 3,112 kutoka 3,155. Dizeli imeshuka hadi Sh 3,070 kutoka Sh 3,354.

Arusha, petroli imepanda hadi Sh 3,247 kutoka Sh 3,120 na dizeli imepungua hadi Sh 3,211 kutoka Sh 3,252