Bei ya mafuta yazidi kupaa

0
216

Bei ya mafuta nchini imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Julai 2022.

Kwa bei hizo mpya zilizoanza kutumika hii leo, petroli imepanda kwa shilingi 190 kwa kila lita, dizeli imepandq kwa shilingi 179 kwa kila lita na mafuta ya taa yamepanda kwa shilingi 323 kwa kila lita kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imeeleza kuwa, bei ya rejareja mkoani Dar es Salaam ni shilingi 3,410 kwa lita moja ya petroli na shilingi 3,322 kwa lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda na kufikia shilingi 3,765 kwa lita.

Petroli imepanda kwa shilingi 190 kwa kila lita ambapo mwezi uliopita wa Julai iliuzwa shilingi 3,220, shilingi 179 kwa kila lita ya dizeli ambayo mwezi uliopita iliuzwa shilingi 3,143 huku mafuta ya taa yakipanda kwa shilingi 323 kwa lita ambako mwezi uliopita yaliuzwa shilingi 3,442.

Kwa mujibu wa EWURA, bei hizo mpya zimejumuisha ruzuku ya shilingi bilioni 100 iliyotolewa na serikali vinginevyo lita ya petroli ingeuzwa shilingi 3,630 na dizeli shilingi 3,734 mkoanii Dar es Salaam.