Barty atinga fainali

0
514

Mwanadada Ashleigh Barty wa Australia ametinga hatua ya fainali ya mashindano ya wazi ya Miami (Miami Open) yanayoendelea nchini Marekani baada ya kuibuka na ushindi wa seti Mbili kwa bila dhidi ya Anett Kontaveit wa Estonia.

Barty amemshinda Kontaviet kwa ushindi wa 6-3 na 6-3 na kutinga fainali ambayo inakuwa hatua kubwa kuwahi kufikiwa na mwanadada huyo kwenye mashindano ya mchezo wa Tenisi tangu alipoanza kucheza mchezo huo.

Barty  mwenye umri wa miaka 22,  aliwahi kushinda ubingwa wa mashindano hayo ya Miami kwa wachezaji wawili wawili yaani womens doubles mwaka  2018 akiwa na Coco Vandeweghe wa Marekani  na anasema mchezo wa robo fainali dhidi ya Kontaviet haukuwa mrahisi.

Katika fainali,  Barty atakutana na mshindi kati ya Simona Halep wa Romania au Karolin Pliskova ambao wanachuana katika nusu fainali ya mwisho.