Baraza la Vijana Zanzibar limemponmgeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utendaji kazi wake huku likisisitiza kuwa kundi la vijana lina imani kubwa na wanamtakia heri na kumuunga mkono katika utendaji kazi wake.
Aidha, baraza hilo limempongeza Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mariam Mwinyi kwa uzinduzi wa taasisi hiyo ambayo itaboresha maisha ya Wazanzibar.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa baraza hilo, Yunus Juma Ali wakati akipokea taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka 2022 ya utendaji wa kamati za baraza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita.
Katika taarifa za kamati, changamoto mbalimbali zimebainishwa kuwakabili vijana hasa wenye ulemavu ukwemo uchache wa watafsiri wa lugha ya alama, gharama kubwa za upatikanaji wa fimbo nyeupe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Mazingira na Mahitaji Maalum, Jamila Borafia amewasisitiza vijana kujiunga kwenye baraza hilo ili kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza, huku akiwaasa kujituma na kuondoa tamaa ya kifedha.