Hakuna wizi wa bando

0
255

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba uchunguzi uliofanya ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) umebaini kuwa hakuna wizi wa vifurushi vya mawasiliano ya simu unaofanywa.

Waziri Nape amesema, kuna changamoto mbili kubwa kwenye matumizi ya simu janja ambapo, kwanza, mtumiaji anaweza kujiunga kifurushi cha intaneti, licha ya kuwa hatumii simu, kikapungua au kuisha kwa sababu kuna programu zinazoendelea kujiendesha kwenye simu.

Ametaja changamoto ya pili kuwa matumizi ya ‘hotspot’ ambapo uchunguzi wa TCRA umebaini kuna watu wamekuwa wakitumia huduma ya hotspot kwenye simu za watu wengine, hivyo kupelekea vifurushi vyao kuisha kwa wakati.

Waziri ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma na kueleza kwamba elimu zaidi inahitajika juu ya matumizi ya intaneti na simu janja, na kwamba, hakuna wizi wowote unaofanywa.