Bandari ya Mtwara yaongezewa mitambo

0
193

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeanza utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya uwekezaji mkubwa wa vifaa katika bandari ya Mtwara ili kazi ifanyike kwa ufanisi zaidi.

Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Nicodemus Mushi amesema mitambo miwili ya kubeba mizigo imewasili katika bandari ya Mtwara ili kuongeza nguvu na uwezo wa kiutendaji katika bandari hiyo.

Amesema mitambo hiyo mmoja utakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 na mwingine kubeba tani 63.

Mitambo hiyo miwili, mmoja umetolewa bandari ya Tanga na mwingine umetoka bandari ya Dar es Salaam.