Bandari ya Dar, kiungo muhimu katika uchumi wa nchi

0
102

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema asilimia 40 ya mapato ya Serikali yanatokana na bandari, na hivyo kuifanya kuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuimarisha uchumi wa sekta nyingine jambo linaloleta matokeo chanya ya ujenzi wa miradi ya kimkakati hapa nchini.

Mrisho ametoa kauli wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari wanaofanya kazi kwenye mikoa yenye bandari nchini.

Amesema moja Kati ya mradi wa kimkakati unaoendelea hapa nchini kwa kutumia mapato ya bandari ni pamoja na ujenzi wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Aidha, ameongeza kuwa maboresho yaliyofanyika yameongeza ufanisi bandarini hapo ambapo wanahudumia zaidi ya magari 2,000 kila siku, asilimia 60 kati ya hayo huenda nchi jirani.