Bandari Kavu Kwala kutumika Kimataifa

0
368

Meneja Miliki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Alexander Ndibalema amesema eneo la Bandari Kavu ya Kwala iliyopo mkoani Pwani lenye ukubwa Hekta 502 limefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi na kutenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya nchi jirani ambazo Tanzania inashirikiana nazo katika biashara kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema mpaka sasa nchi nane tayari zimegawiwa Hekta 100, nchi ambazo ni Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia, Uganda, Malawi, Zimbabwe na Sudan Kusini.

Ndibalema amesema ushirikiano wa kibiashara na nchi hizo utasaidia kupunguza wingi wa mizigo pamoja na msongamano wa maroli ndani ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa asilimia 60 ya mizigo itapelekwa Bandari Kavu ya Kwala.

Baadhi ya nchi zimeshaanza utekerezaji katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, nchi ambazo zimepeleka Wataalamu na Wakandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.