Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Battle leo Machi 10, 2023 ametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea shughuli za uendeshaji, kufahamu historia ya TBC pamoja na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Ayub Rioba Chacha.
Akiwa TBC Balozi Battle pamoja na mambo.mengine, ameshiriki katika kipindi maalum, kilichorushwa Mbashara kupitia TBC1 kilicholenga kuzungumzia uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Marekani.
Balozi huyo wa Marekani nchini ameeleza kufurahishwa na namna TBC inavyotekeleza majukumu yake na inavyozidi kupiga hatua katika matumizi ya teknolojia hasa kupitia studio zake za kisasa.