Balozi Karume ajitosa Urais Zanzibar

0
362

Balozi Ali Karume amechukua fomu kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja, Balozi Karume amesema kuwa endapo atateuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais na baadaye kushinda kiti cha Urais wa Zanzibar ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake.

Pia ameahidi kuimarisha muungano kwa manufaa ya Wanzania wa pande zote mbili za Muungano huo.

Balozi Karume ambaye kwa sasa ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, pia amewahi kuwa Balozi wa Tanzania katika nchini mbalimbali duniani.