Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limemchagua Deodatus Balile kuwa Mwenyekiti wake kwa kura 57, dhidi ya kura 22 alizopata mshindani wake Neville Meena.
Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani Morogoro, unapofanyika mkutano wa TEF.
Kabla ya uchaguzi huo, Balile alikuwa akikaimu nafasi hiyo, huku Meena akiwa Katibu wa TEF.