Bajeti ya Serikali ya Tanzania 2019/20

0
483

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kuwasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 bungeni jijini Dodoma.

Matunda ya kikao cha Rais Dkt. John Magufuli na wafanyabiashara yameonekana baada ya serikali kuamua kupunguza tozo mbalimbali za wafanyabiashara.

Katika bajeti hiyo, kodi ya taulo za kike imerejeshwa.

Nywele bandia kutoka nje na zinazotengenezwa hapa nchini zimeongezewa kodi.

Watumishi wa Mamlaka ya Mapato wakaonywa kuhusu kufunga biashara kwa kushinikiza mtu kulipa kodi bila kibali cha Kamishna wa Mamlaka ya mapato nchini.

Jumatatu wiki ijayo wabunge wataanza kuchangia bajeti ya jumla ya shilingi Trilioni 33.1