Bajeti ya serikali kwa mwaka 2020/2021 yapita

0
296

Wabunge wamepitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 ya jumla ya shilingi Trilioni 34.88.

Bajeti hiyo imepitishwa kwa kura 304 za ndio kati ya kura 371 zilizopigwa na wabunge waliokuwepo bungeni jijini Dodoma.

Juni 11 mwaka huu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango aliwasilisha hotuba ya bajeti bungeni na baadaye kujadiliwa na Wabunge mbalimbali.