Bajeti ya Bil 350/- Ofisi ya Waziri Mkuu yapita

0
334

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 15, 2024 limepitisha kiasi cha shilingi 350,988,412,000 kwa ajili ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Katika bajeti hiyo, shilingi 146,393,990,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 204,594,422,000 ni kwa matumizi ya maendeleo.

Vilevile Bunge limeidhinisha jumla ya shilingi 181,805,233,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, shilingi 172,124,423,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 9,680,810,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.