Million 307.933 Kunufaisha Wanawake Vijana na Walemavu Bagamoyo ili kujikwamua Kiuchumi huku ikiwa ndio pesa kiasi kikubwa zaidi kuliko miaka yote.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji Shauri Selenda Amesema Watatoa Mikopo zaidi ya milioni 307.99 inayotokana na Asilimia 10% ya Mapato ya Halmashauri ikiwa ndio mara ya kwanza kutoa Kiasi kikubwa ili kisaidie kuinua Uchumi wa Vijana, Wanawake na Walemavu.
Selenda Amesema Pesa hiyo inatolewa kutokana na Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aidha Ameomba Vijana kutumia Pesa hiyo vizuri na kurejesha kwa wakati ili na wengine wanufaike.