Badilisheni muundo kada ya uuguzi

0
132

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ametoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kumaliza changamoto ya kubadilisha muundo kwa watumishi wa kada ya uuguzi kupandishiwa mishahara na kupandishwa vyeo pindi wanapotoka kujiendeleza kimasomo.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo mkoani Tanga wakati akifunga mafunzo ya 51 ya Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA).