Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewahakikishia wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa, hakuna mtu wa kuwakamata na kwamba wataondoka salama mkoani humo.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Wanawake wa CHADEMA yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Babu amesema, chini ya uongozi wake hakuna mtu atakayekamatwa akiwa mkoani humo.
“Napenda kumtoa hofu mwenyekiti wa mkoa, yaliyopita si ndwele tugange yajayo, Mheshimiwa Rais chini ya uongozi wangu hakuna mtu atakayekamatwa.” amesema Babu