Babu: Madereva kuweni makini

0
276

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Babu ameyasema hayo wilayani Rombo alipoongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga miili ya watu 12 waliofariki dunia Februari 3 mwaka huu wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Babu amesema iwapo madereva watafuata sheria watasaidia kupunguza ajali zisitokee mara kwa mara na kugharimu maisha ya watu.

“Niwaombe viongozi wa jeshi la polisi hebu tujitahidi huko barabarani kwani kazi ya udereva ni kazi ya taaluma kama taaluma nyingine, tumeweka vibao lakini bado madereva hawaelewi wala hawasikii.” amesema mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro.