Mtoto wa miezi mitano, Leonard Kubilu, amefariki baada ya kupigwa na baba yake mzazi, Kubilu Bayege, mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa, Mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mauaji ya mtoto huyo yametokea jana, chanzo ikiwa ni ugomvi wa kifamilia.
Mama mzazi wa marehemu, Riziki Leonard, amesema mumewe alimpiga mtoto makofi pamoja na kumchapa kwa mkanda wa suruali katika maeneo mbalimbali mwilini mwake baada ya kuona (mtoto) analia usiku.
Kwa upande wake Mtendaji wa Mtaa wa Kilimahewa, Marko Chuma, amesema mtuhumiwa wa mauji hayo alitoroka baada ya kutekeleza mauji.