Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia wilayani Kilosa mkoani Morogoro baada ya kuungua kwa moto usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha vifo hivyo ni baba kuichoma moto familia hiyo na yeye akiwemo.
Baadhi ya majirani wamesema huenda hatua hiyo imesababishwa na ugumu wa maisha.
Waliokufa kwenye tukio hilo ni baba wa famlia hiyo, Amani malekela (72) na watoto wake Habibu Amani (10), Sadick Aman (8) na Bahati Amani (5).