Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, – Job Ndugai ameziagiza Kamati zote za Bunge zilizokua kwenye ziara katika maeneo mbalimbali nchini kurejea jijini Dodoma.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema kuwa, agizo hilo linafuatia mlipuko wa virusi vya corona
Amesema shughuli za ufuatiliaji miradi na kazi za uchambuzi wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021, katika ngazi ya kamati kwa kiasi kikubwa zitafanyika kwa njia ya mtandao ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.
Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, mkutano wa Bunge utaendelea kama ilivyopangwa kuanzia machi 31 mwaka huu, ingawa kutakuwa na mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji.
Amewataka Wabunge wote kuchukua tahadhari dhidi virusi vya corona wanapokua Dodoma, ikiwa ni pamoja na kutojichanganya kwenye makundi ya mitaani.