Azam wakataliwa kurusha mechi ya Yanga

0
371

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Rivers United ya Nigeria na Yanga SC ya Tanzania hautorushwa mbashara baada ya Azam Media kukataliwa kurusha matangazo kwa njia ya video na sauti.

“Tunasikitika kuwaarifu kwamba, hatutaweza kuwaletea matangazo ya moja kwa moja ya mchezo wa CAF Champions League kati ya Rivers United na Yanga SC,” wameeleza Azam.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, Rivers United uliondoka na ushindi wa goli 1-0, hivyo Yanga inahitaji kupindua meza ugenini ili ibaki kwenye mashindano hayo.