Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtengua Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema, Mhandisi Robert Lupoja na kumteua Mhandisi Sadala Hamis katika nafasi hiyo.
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Sadala alikuwa mtumishi katika Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) DDCA.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso, ameivunja bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema.