Aweso atembelea mitambo ya maji Ruvu

0
160

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini na kupokea taarifa ya hali ya upatikanaji maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Katika ziara hiyo Waziri Aweso amefika eneo maalum la upimaji wa kina cha maji na kujionea hali ilivyo akisisitiza kuwa ni suala la muda hali itarejea kama kawaida hasa kukiwa na dalili ya mvua kuanza kunyesha.

Aidha Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya maji yanayopatikana na kutoa wito kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia ratiba za mgao wa maji zilizowekwa ili kila mwananchi apate huduma ya maji.

Katika ziara hiyo Waziri Aweso amefuatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange na Mkurugenzi wa Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Elibariki Mmasy.