Aweso ataka tathmini changamoto ya maji

0
210

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza kuundwa timu ya wataalam itakayofanya tathmini ya changamoto ya maji, inayoikabili halmashauri ya Korogwe Mji mkoani Tanga.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake wilayani Korogwe, ziara iliyolenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya uhaba wa maji uliopo kwa sasa kwenye halmashauri hiyo .

Aidha ameagiza timu hiyo ya wataalam itakayofanya tathmini ya changamoto ya maji
ikamilishe kazi hiyo ndani ya kipindi cha siku saba na kutoa majibu ya hatua zitakazochukuliwa ili kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hiyo.

Wilaya ya Korogwe inahitaji shilingi Milioni 825.3 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maji ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa visima saba.