Aua watoto kwa madai ya ugumu wa maisha

0
246

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia mkoani Geita, baada ya mama yao mzazi kuwanywesha sumu na kisha  yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika kijiji cha Mwabagaru wilayani Chato, huku akimtaja mama wa watoto hao kuwa ni Veronica Gabriel mwenye umri wa miaka 30 ambaye amenusurika kifo baada ya kunywa sumu hiyo.
 
Amesema Mama huyo mwenye watoto watano, aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao ndio waliofariki dunia.
 
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe, watoto wengine wamelazwa katika kituo cha afya cha  Bwanga pamoja na mama yao ambaye amewekwa chini ya ulinzi.