ATCL yaanza rasmi safari za China leo

0
514

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) leo alfajiri imezindua rasmi safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou nchini China.

Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Jengo Namba 3 la abiria (terminal 3) katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi. Ladislaus Matindi.

Kwa mujibu wa ATCL, safari kati ya Dar es Salaam na Guangzhou itatumia saa 11 na zitakuwa safari pekee za moja za moja kwa moja kati ya maeneo hayo mawili.

Ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na tani 20 za mizigo itakuwa ikifanya safari zake mara moja kila baada ya wiki mbili huku ikitumia.

Matindi amesema wataendelea kutanua wigo kutokana fursa zinazojitokeza.

Kwa upande wake Waziri Chamuriho amesema serikali itaendelea kuiboresha ATCL lakini amewataka watendaji wake kutoa huduma bora kwa abiria.

Licha ya Kibali kutolewa Januari 20 cha kusafirisha abiria kutoka Dar es Salaam hadi Guangzhou, janga la virusi vya corona lilisababisha ATCL kushindwa kuanza safari hizo kwa wakati.

Tangu mwaka 2015 serikali imewekeza nguvu katika kufufua kampuni hiyo ambapo jitihada hizo ni pamoja na kununua ndege, kukarabati na kujenga viwanja vya ndege na kuongeza rada za kuongozea ndege ili kuziwezesha ndege za shirika hilo kufika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.