Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas amesema kuwa, mtu yeyote atakayebainika kuhujumu suala la ndege mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini atawajibishwa kwa mujibu wa sheria ya nchi ya uhujumu uchumi.
Dkt Abbas ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari ambapo pia amezungumzia masuala mbalimbali yanayolihusu Taifa.
Pia amewaambia Waandishi wa habari kuwa utafiti uliofanywa kwa pamoja na Taasisi ya Trasparency International na ile ya Afro Barometer umeonyesha Tanzania kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya vitendo rushwa.