Diwani wa kata ya Chanika wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Adballa Chihumpu amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo akidaiwa kutoa maneno ya udhalilishaji dhidi ya mwekezaji Stanley Liakindi anayetuhumiwa kuchukua eneo la wazi la shule ya msingi Chanika na hivyo kuzusha mgogoro kati yake na wananchi wa eneo hilo.
Shauri hilo limetajwa mahakamni hapo kwa mara ya kwanza na Hakimu Martha Mabapala ambaye ameliahirisha hadi Aprili 22, 2024 litakapotajwa tena kutokana na Hakimu aliyepangwa kulisikiliza Veronica Siao kutokuwepo mahakamani hapo.
Katika shauri hilo mlalamikaji ambaye ni mwekezaji Stanley Liakindi anadai fidia ya shilingi Milioni 150 kuroka kwa diwani huyo wa kata ya Chanika, Adballa Chihumpu ambaye anadai alimtolea maneno yenye udhalilishaji.