Wakristo nchini wamehimizwa kujijengea tabia ya kusoma maandiko matakatifu ili kuimarisha imani zao na kuwa mashahidi wa kweli wa Mungu na Kristo mfufuka.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yude Thadeus Rwai’chi wakati wa ibada ya Misa Takatifu ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika kitaifa katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Askofu Rwai’chi ameongeza kuwa fumbo la Pasaka ni sehemu ya kumfanya mkristo kuwa kiumbe kipya cha Mwenyezi Mungu mahali popote.
“Petro mtume alitangaza ushahidi wa Yesu Kristo mfufuka bila kujali macho ya waliomzunguka hivyo Wakristo popote walipo wanatakiwa kushuhudia ufufuko huo kwa imani thabiti bila kujali tofauti zao.
Aidha Askofu Rwai’chi amesema ni vyema Wakristo kutumia sherehe za Pasaka kama sehemu ya kuwakumbuka wenye mtahitaji maalumu wakiwemo masikini na wagomjwa.
“Wabatizwa wanaitwa kuwa mashahidi wa Kristo mfufuka kama ambavyo Petro alivyofanya mbele ya mitume wa Yesu,” amesisitiza Askofu Rwai’chi.
Sherehe ya Pasaka ni kumbukumbu ya kufufuka kwa Kristo Yesu baada ya kusulubiwa msalabani na kuzikwa Ijumaa Kuu.