Askofu Afwilile awekwa wakfu

0
169

Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mashariki Lawi Afwilile amewataka Watanzania kuungana na Kanisa hilo kusaidia Serikali ku tekeleza na kupanga mipango ya maendeleo kwa watu wote kupitia sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti mwaka 2022.

Askofu Afwilile amesema hayo wakati akitoa neno la shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kanisa hilo katika ibada maalum iliyofanyika Chamanzi, Mkoani Dar es Salaam.

“Kutoshirki kwenye sensa ya watu na makazi ni ishara ya kuisaliti Serikali katika juhudi za kupanga mipango ya maendeleo kwa kila mwananchi”Amesema Askofu Afwilile.

Pia ameupongeza uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuitangaza nchi kupitia Filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Aidha ameushukuru uongozi wa Kanisa hilo kwa kumuamini na kumteuwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mashariki na kuwahakilishia utumishi uliotukuka.

Amesema atafanya kazi ya Mungu kwa kushirikiana na watumishi wengine wa Kanisa hilo na wadau wengine kwa Maendeleo ya Kanisa na jamii inayowazunguka.

Pamoja na mambo mengine askofu Afwilile ameihakilishia Serikali ushirikiano wa dhati katika kupiga vita vitendo vya ukatili kwenye jamii ikiwa ni pamoja kupiga vita vitendo vya rushwa kwa Ustawi wa taifa.