Askari Polisi watatu wafariki, tisa wajeruhiwa

0
542

Askari Polisi watatu wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya gari dogo la polisi walilokuwa wakisafiria kwenda lindoni kugongana na basi la abiria la Sharom.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 12 asubuhi katika daraja la Mto Ruhiji mjini Njombe ambapo majeruhi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Akizungumzia ajali hiyo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe, Kibena Alto Mtega amesema imehusha watu 12, na majeruhi hao wameanza kutibiwa.