Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu linazozifanya na namna linavyoshiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka TPDC Marie Mselem katika maonesho ya bidhaa na huduma yanayofanyika uwanja wa CCM Sabasaba mkoani Njombe kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Aprili 2 mwaka huu.
Amefafanua kuwa asilimia sitini ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi asilia.
“Tumefurahi na tumepata mwitikio mkubwa sana, na wameelewa vitu ambavyo TPDC wanafanya kama Shirika lao la Mafuta. Pia wameelewa kwamba asilimia sitini ya umeme unaozalishwa hapa nchini unatokana na gesi asilia”- amesema Marie.
TPDC ni miongoni mwa mashirika yanayoonesha bidhaa na huduma zao kwa Wananchi kuelekea uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru.