Arudwasha Titika, mkazi wa kijiji cha Alaitore kilichopo ndani ya hifadhi Ngorongoro mkoani Arusha amefariki dunia baada kushambuliwa na tembo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtu huyo alishambuliwa na tembo wakati akitafuta kuni akiwa na wenzake ndani ya hifadhi hiyo tarehe 9 mwezi huu majira ya mchana.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Masejo amewataka Wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuchukua tahadhari na kuhakikisha wanafuata maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika.