Asanteni sana TBC

0
289

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, amelishukuru Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa maboresho ambayo limeyafanya na hivyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

“Nichukue nafasi hii kuwashukuru wote lakini kipekee niwashukuru TBC kwa kuendelea kutanua huduma zao kila kona ya nchi yetu, asanteni sana chini ya Mwenyekiti wa bodi wanafanya vizuri sana,” amesema Waziri Nape

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) kwenye kiwanja cha Kasim Majaliwa Majaliwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.