Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amesema, katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, mkoa huo umefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali ikiwa ni pamija na afya , elimu, miundombinu na michezo.
Mongella amesema katika afya wamefanikiwa kujenga majengo ya utoaji wa huduma za afya kwa wilaya zote mkoani humo.
Katika Elimu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuthubutu kutoa fedha za UVIKO – 19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mongella alikuwa akitoa tathmini ya .mkoa wa Arusha katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.