Arumeru wafungua kiwanda cha barakoa

0
215

Wilaya ya Arumeru leo imezindua kiwanda kidogo kitakachokuwa kikizalisha Barakoa kwa ajili ya watumishi wa sekta ya afya katika wilaya hiyo.

Akizindua kiwanda hicho Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema kiwanda hicho kidogo kitakuwa ni mali ya Serikali na kipo ndani ya hospitali ya Halmashauri ya Meru Tengeru.

” Tunatengeneza barakoa kwa ajili ya watumishi wetu wote wa sekta ya afya kwa vituo vyetu vya afya na zahanati,” amesema Muro.