Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amesema mfumo wa anwani za makazi una umihimu katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na yale ya Taifa
Mhandisi kundo ameyasema hayo mkoani Simiyu katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji wa mkoa huo kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za wakazi.
“Manufaa ya mfumo wa anwani za makazi yameelezwa wazi kwamba unarahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishaji wa huduma ama bidhaa hadi mahali stahiki; unaimarisha ulinzi na usalama; unawezesha kufanyika kwa biashara Mtandao, unaongeza ajira; na unawezesha kufanyika kwa tija kwa mipango na tafiti.” amesema Mhandisi Kundo