Na Sauda Shimbo
ROMBO
Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja (jina linahifadhiwa) kwa tuhuma za mauaji ya dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Oscar Kiondo, mkazi wa Kijiji cha Holili wilayani Rombo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea katika baa ya Afrikasana wilayani humo ambapo mtuhumiwa alimchoma Oscar kwa kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo chake.
Kamanda Maigwa amesema chanzo cha ugomvi huo ni ulevi wa pombe kati ya marehemu na mtuhumiwa wakiwa wanakunywa pombe kwenye baa hiyo.
Amesema marehemu Oscar amefariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali ambapo mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Faraja iliyoko kagika Mji Mdogo wa Himo.