Amani yasisitizwa sikukuu ya Eid

0
198

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa rai kwa Waumini wa dini ya Kiislam nchini na Watanzania wote kuendelea kuvumiliana na kushirikiana,  pamoja na kulinda amani ya nchi.
 
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa rai hiyo katika Baraza la Eid El Adha lililofanyika kwenye msikiti wa Mtoro, Ilala mkoani Dar es Salaam.
 
Amesema kila Mtanzania anapaswa kutambua kwamba ana mchango mkubwa katika kutunza amani, hivyo ni vema akafanya hivyo kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.
 
Waziri Mkuu amesema amani ni jambo muhimu katika kuhamasisha maendeleo ya Taifa lolote duniani, na kama Tanzania inataka kupiga hatua zaidi za kimaendeleo suala la amani ni jambo la msingi.