Aliyepandikizwa figo ya nguruwe afariki

0
200

Hospitali Kuu ya Massachusetts iliyopo Boston nchini Marekani imesema Rick Slayman mwenye umri wa miaka 62 amefariki dunia ikiwa imepita miezi mwili tu baada ya kufanyiwa upasuaji na kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba.

Slayman ambaye ni mwanaume wa kwanza kupandikizwa figo ya nguruwe, alitarajiwa kuleta matumaini kwa wagonjwa wengi wenye maradhi ya figo duniani.

Alikuwa akisumbulia na maradhi ya figo ambapo alifikia hatua ya mwisho ya ugonjwa huo kabla ya kufanyiwa upasuaji huo na kupandikizwa figo ya nguruwe Machi 16 mwaka huu.

Hata hivyo hospitali hiyo ya Massachusetts imesema hakuna dalili kwamba kifo cha mwanaume huyo ambacho kimetokea ghafla ni matokeo ya upandikizaji aliofanyiwa.