Aliyekuwa Mkurugenzi Temeke afikishwa mahakamani Kisutu

0
140

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Lusubilo Mwakabibi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili kusomewa mashitka yanayomkabili.

Mwakabibi amefikishwa mahakamani hapo baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea miradi iliyopo katika manispaa hiyo nakubaini ubadhirifu wa fedha za miradi uliofanyika wakati mkurugenzi huyo akiwa madarakani, na kuviagiza vyombo vya sheria kumchukulia hatua.

Mwakabibi ambaye amefikishwa mahakamani hapo na maafisa wa TAKUKURU, bado yuko chini ya ulinzi akisubiri kusomewa mashitaka yaliyoko mbele yake.