Akamatwa Na Kipande Cha Jino La Tembo

0
251

Mkazi mmoja  wa kata ya Mpepai tarafa ya Mbinga Mjini mkoani Ruvuma amekamatwa akiwa na kipande kimoja cha jino la tembo chenye uzito wa gramu 722 lenye thamani ya shilingi milioni 34 (34,725,000/=).

Kamanda wa Polisi wa mkoani Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saimon Maigwa amesema Jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori wa pori la akiba la Liparamba lililopo wilaya ya Mbinga wamefanikiwa kumkataa mtu huyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi, Kamanda wa Polisi wa mkoani Ruvuma, Saimon Maigwa amesema kipande hicho cha jino la tembo kimekamatwa saa tisa usiku wa kuamkia Juni 11, mwaka huu.

Pia Kamanda Maigwa amesema mfanyabiashara na mkazi wa Njombe amekamatwa na bangi kilo tano.

Katika tukio jingine Kamanda Maigwa amesema Issa Yahaya mwenye umri wa miaka 33 amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kulipa fidia ya shilingi milioni mbili  baada ya kumdhalilisha mwanafunzi mwenye umri miaka 16 na kumsababishia ujauzito.